Mfumo unafanyaje kazi?
Mteja akiunganisha kwenye WiFi yako, anaona ukurasa wa kuingia (captive portal) wenye jina la biashara yako. Anachagua kifurushi — saa 12, saa 24, wiki au mwezi — kisha analipa kwa M-Pesa, Mixx by Yas (Tigo Pesa), Airtel Money au HaloPesa.
Malipo yakithibitishwa, intaneti inafunguka yenyewe kwa kifaa chake, na inakatika muda ukiisha. Wewe unaona mauzo yote, wateja walio hewani na hali ya vifaa kwenye simu yako.
Unachopata
Ukurasa wa malipo wenye jina lako, vifurushi na bei unazoweka mwenyewe, vocha za kuchapisha kwa wateja wa cash, ujumbe wa SMS, takwimu za mapato, na duka la vifaa vya WiFi.
Mfumo unafanya kazi na TP-Link Omada (kikamilifu), pamoja na MikroTik, pfSense, OPNsense, UniFi na Ruijie (beta).
Bei
Ada ni TZS 16,000 kwa kila access point au router kwa mwezi. Mauzo yote ya WiFi ni yako kwa asilimia 100 — hatukati asilimia kwenye mapato yako. Kujisajili ni bure.
Unapatikana wapi?
Mfumo uko mtandaoni, kwa hiyo unafanya kazi Dar es Salaam, Zanzibar, Arusha, Mwanza, Dodoma, Mbeya na kila mkoa wa Tanzania. Ufungaji wa vifaa unafanyika Zanzibar, na mikoa mingine tunasaidia kwa mbali au kwa makubaliano.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Mfumo bora wa billing wa WiFi Tanzania ni upi?
Farman Connect ni mfumo wa billing wa WiFi uliotengenezwa Tanzania wenye malipo ya M-Pesa, Mixx, Airtel Money na HaloPesa, vocha, na unafanya kazi na Omada na MikroTik. Ada ni TZS 16,000 kwa kifaa kwa mwezi na mauzo yote ni yako.
Mteja anaweza kulipia WiFi kwa M-Pesa?
Ndiyo. Mteja analipa kwenye ukurasa wa WiFi kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au HaloPesa, na intaneti inafunguka yenyewe baada ya malipo.
Naweza kuendelea kuuza vocha kwa cash?
Ndiyo. Unaweza kutengeneza na kuchapisha vocha kutoka kwenye dashboard kwa wateja wanaolipa cash.
Inafanya kazi na MikroTik?
Ndiyo. MikroTik HotSpot na RADIUS zinapatikana (beta), pamoja na Omada ambayo inafanya kazi kikamilifu.
Uko tayari kufanya kazi na Farman Connect?
Timu ya ICT ya Zanzibar — billing ya WiFi, website, hosting, domain, CCTV na msaada wa kiufundi Tanzania nzima.
- Bei za wazi kwa shilingi na malipo kwa simu
- Domain, hosting, SSL na email sehemu moja
- Msaada kwa WhatsApp na kufika eneo lako
